Somalia
Jamhuri ya Somalia Jamhuuriyadda Federaalka Soomaaliya | |
---|---|
Kaulimbiu: Qaranimo, Cadaalad, Midnimo (Kisomali: "Utaifa, Haki, Umoja") | |
Wimbo wa taifa: Qolobaa Calankeed | |
Mji mkuu na mkubwa | Mogadishu |
Lugha rasmi | Kisomali, Kiarabu |
• Rais | Hassan Sheikh Mohamud |
• Waziri Mkuu | Hamza Abdi Barre |
Historia | |
• Uhuru | 1 Julai 1960 |
• Muungano na Somaliland | 1 Julai 1960 |
• Katiba ya sasa | 1 Agosti 2012 |
Eneo | |
• Jumla | km2 637,657 km² (ya 43) |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | ▲ 18,143,378 |
• Msongamano | 27.2/km²/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2023 |
• Jumla | ▲ $34.03 bilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $2,060 |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2023 |
• Jumla | ▲ $12.8 bilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $775 |
HDI (2022) | ▬ 0.380 chini |
Gini (2017) | 36.8 |
Sarafu | Shilingi ya Somalia (SOS) |
Majira ya saa | UTC+3 (EAT) |
Upande wa magari | Kulia |
Msimbo wa simu | +252 |
Jina la kikoa | .so |
Somalia,(kwa Kisomali: Soomaaliya) rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi katika Afrika ya Mashariki, iliyoko kwenye Pembe ya Afrika. Inapakana na Ethiopia magharibi, Djibouti kaskazini-magharibi, Kenya kusini-magharibi, na imezungukwa na Bahari ya Hindi mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 17.1, ikiwa ya 70 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Mogadishu. Somalia imegawanyika katika majimbo sita ya shirikisho. Inajulikana kwa pwani yake ndefu zaidi barani Afrika na changamoto zake za kisiasa na kiusalama kutokana na miongo ya migogoro ya ndani.
Jiografia

Historia

Ukoloni wa Italia
Kuanzia mwaka 1888 Italia ilijipatia mikataba ya ulinzi na masultani mbalimbali waliotawala maeneo madogo kwenye Pembe ya Afrika. Walitangulia 1889 na sultani ya bandari ya Hobyo na mtawala wa usultani wa Majerteen.
Mwaka 1892 Usultani wa Zanzibar ulikodisha bandari ya Banadir kati ya Mogadishu hadi Brava kwa Italia. Mwaka 1905 Italia ilinunua eneo hili kutoka Zanzibar na kulitangaza kuwa koloni na Mogadishu kuwa mji mkuu.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waitalia walikabidhiwa na Uingereza eneo la Kismayu. Walilitawala kwa jina la "Oltre Giuba" (ng'ambo ya mto Juba) na kuliunganisha na Somalia ya Kiitalia tarehe 30 Juni 1926.
Wakati uleule waliamua kumaliza hali ya sultani za Majarteen na Hobyo kuwa nchi lindwa na kuzifanya sehemu kamili za koloni. Mipango hiyo ilisababisha vita kali ya miaka miwili kwa sababu masultani waliona mikataba yao ya ulinzi ilivunjwa wakapinga jeshi la Italia.
Mwaka 1936 Somalia ikaunganishwa na Ethiopia kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kiitalia.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia makoloni ya Italia yalivamiwa na Uingereza uliotawala Somalia tangu 1941.
Mwaka 1949 Somalia ilirudishwa mikononi mwa Italia ilisimamie kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.
Ukoloni wa Uingereza
Uingereza uliingia katika eneo hili baada ya Misri kuondoka mwaka 1885 kwa kushindwa na jeshi la Mahdi huko Sudan. Uingereza uliingia kwa sababu iliona umuhimu wa kutawala pande zote mbili za Bab el Mandeb ikihofia uenezaji wa nchi nyingine za Ulaya, hasa Ufaransa iliyokuwa na koloni la kwanza ya Ubuk (Obok) katika Jibuti ya leo tangu 1862. Pamoja na hayo Waingereza walitegemea kununua nyama kwa ajili ya mji wa Aden na meli zilizopita hapo kati ya Uhindi na Ulaya.
Somaliland ilitawaliwa awali kama mkoa wa Uhindi wa Kiingereza ikawa baadaye chini ya wizara ya makoloni huko London.

Hata kama Uingereza haukuwa na nia ya kuingilia mno maisha ya wenyeji ulikutana na upinzani mkali kuanzia mwaka 1899 kutoka kwa kiongozi wa dini Diiriye Guure, aliyeitwa na Waingereza "Mullah majununi". Waingereza walijibu kwa ukatili katika vita vya miaka 20 iliyoua takriban theluthi moja ya wakazi wote wa eneo.
Mwishowe Uingereza iliweza kumaliza upinzani kwa teknolojia mpya ya eropleni za kijeshi zilizotumia mabomu na bunduki za mtombo kutoka angani kwa mara ya kwanza katika Afrika.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia eneo likatwaliwa na Italia katika Agosti 1940 lakini lilichukuliwa tena na Uingereza katika Machi 1941.
Uhuru
Mwaka 1960 utawala wa kikoloni ulikwisha na Somalia ikapata uhuru wake, ikiunganisha makoloni mawiliː la Waitalia (kusini) na la Waingereza (kaskazini).
Baada ya mwaka 1991 nchi ya Somalia ilibaki haina serikali wala umoja wa taifa, bali iligawiwa na wakereketwa na wanamgambo wa ukoo na eneo, hasa Somaliland, Puntland na Galmudug upande wa kaskazini.
Katika miaka 2008-2013 ilihesabika kama nchi filisika. Kwa sasa ni nchi dhaifu lakini inaanza kujengwa upya kama shirikisho na kujiandaa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tarehe 4 Machi 2024 imejiunga rasmi na Jumuia ya Afrika Mashariki[1].

Watu
Tazama pia: Orodha ya lugha za Somalia

Wakazi asili wa Somalia ni Wasomali (85%) wa makabila yafuatayo:
Wengine (15%) ni:

Kisomali ndiyo lugha ya kawaida ya wakazi wengi na lugha rasmi pamoja na Kiarabu. Kati ya lugha nyingine zinazotumika nchini, mojawapo ni Kiswahili (lahaja za Chimbalanzi na Kibajuni).
Upande wa dini, 99.8% ni Waislamu, hasa Wasuni. Wakristo hawafikii 0.1%.








Utawala
Maeneo (umoja: gobolka, wingi: gobollada) ya Somalia, ambayo imegawiwa tena katika wilaya, ni 18:
Mkoa | Eneo (km2) | Wakazi | Makao makuu |
---|---|---|---|
Awdal | 21,374 | 1,010,566 | Borama |
Bari | 70,088 | 719,512 | Bosaso |
Nugal | 26,180 | 392,697 | Garowe |
Mudug | 72,933 | 717,863 | Galkayo |
Galguduud | 46,126 | 569,434 | Dusmareb |
Hiran | 31,510 | 520,685 | Beledweyne |
Shebeli wa Kati | 22,663 | 516,036 | Jowhar |
Banaadir | 370 | 1,650,227 | Mogadishu |
Shebeli wa Chini | 25,285 | 1,202,219 | Barawa |
Togdheer | 38,663 | 721,363 | Burao |
Bakool | 26,962 | 367,226 | Xuddur |
Woqooyi Galbeed | 28,836 | 1,242,003 | Hargeisa |
Bay | 35,156 | 792,182 | Baidoa |
Gedo | 60,389 | 508,405 | Garbahaarreey |
Juba wa Kati | 9,836 | 362,921 | Bu'aale |
Juba wa Chini | 42,876 | 489,307 | Kismayo |
Sanaag | 53,374 | 544,123 | Erigavo |
Sool | 25,036 | 327,428 | Las Anod |

Mawasiliano
Mawasiliano ya Jamhuri ya Somalia ilikaribia kuangamia kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini kwa sasa kampuni za binafsi za mawasiliano ya mitambo, zimetwaa karibu miji yote Somalia, na hata kutoa huduma njema kuliko nchi zilizo jirani.
Somalia ni nchi mojawapo Afrika ambayo ina mawasiliano ya bei rahisi zaidi, pengine kwa kuwa Somalia haikuwa na serikali iliyotoza ushuru; (Telecoms thriving in lawless Somalia) Kampuni zinazohudumia watu wa Somalia ni kama:
Tazama pia
- Utamaduni wa Somalia
- Uislamu nchini Somalia
- Waandishi wa Somalia
- Muziki wa Somalia
- Uchumi wa Somalia
- Vita vya Mogadishu
- Mawasiliano nchini Somalia
- Orodha ya kampuni za Somalia
- Jeshi la Somalia
- Usafiri nchini Somalia
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Tanbihi
Marejeo
- Abdullahi, Mohamed Diriye (2001). Culture and Customs of Somalia. Westport, CT: Greenwood Press. ISBN 978-0-313-31333-2.
- Alpers, Edward A. (1976). "Gujarat and the Trade of East Africa, c. 1500–1800". The International Journal of African Historical Studies. 9 (1): 22–44. doi:10.2307/217389. JSTOR 217389.
- Gebru Tareke (2009). The Ethiopian Revolution: War in the Horn of Africa. New Haven, CT: Yale University Press. ISBN 978-0-300-14163-4.
- Laitin, David D. (1977). Politics, Language, and Thought: The Somali Experience. Chicago: University Of Chicago Press. ISBN 978-0-226-46791-7.
- Lecarme, Jacqueline; Maury, Carole (1987). "A Software Tool for Research in Linguistics and Lexicography: Application to Somali". Computers and Translation. 2 (1): 21–36. doi:10.1007/BF01540131.
- Mauri, Arnaldo, Somalia, in G, Dell'Amore (ed.), "Banking Systems of Africa", Cariplo-Finafrica, Milan, 1971, pp. 209–217.[1]
- Samatar, Said S. (1982). Oral Poetry and Somali Nationalism. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-10457-9.
- Schraeder, Peter J. (2006). "From Irredentism to Secession: The Decline of Pan-Somali Nationalism". In Lowell W. Barrington, ed., After Independence: Making and Protecting the Nation in Postcolonial and Postcommunist States (pp. 107–137). Ann Arbor, MI: University of Michigan Press. ISBN 978-0-472-09898-9.
- Shay, Shaul. Somalia in Transition Since 2006. Piscataway, NJ: Transaction Publishers, 2014.
- Warmington, Eric Herbert (1995). The Commerce Between the Roman Empire and India. South Asia Books. ISBN 8121506700.
- Zolberg, Aristide R.; Suhrke, Astri; Aguayo, Sergio (1989). Escape from Violence: Conflict and the Refugee Crisis in the Developing World. New York: Oxford University Press. ISBN 978-0-195-05592-4.
Viungo vya nje
- Wikimedia Atlas of Somalia
- Federal Government of Somalia Ilihifadhiwa 8 Aprili 2015 kwenye Wayback Machine.
- Somalia entry at The World Factbook
- Somalia katika Open Directory Project
- Somalia profile from the BBC News
- Habari, mitandao inayojadili kuhusu Somalia.
- AllAfrica.com - Somalia Habari
- International Freedom of Expression eXchange: Somalia Ilihifadhiwa 14 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Somalia - A Country Study
- Habari za kawaida
- BBC habari barabara - Somalia: Kutoka kwenye mbomoko?
- Somali Planet Networks Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- US State Department - Somalia includes Background Notes, Country Study and major reports
- Better off Stateless: Somalia Before and After Government Collapse
- Watambuzi
- Anarchy and Invention: Vipi Kampuni za Somalia zaweza kufanya biashara bila serikali? Ilihifadhiwa 7 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
Nchi za Afrika | ![]() |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Somalia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |